Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wengi kulalamika miguu kuwaka moto na kuuma sana/kufa ganzi kwa vijana na hata kwa watu wazima.
Miguu kuwaka moto ni ile hali ya kuhisi sehemu ya chini ya miguu inawaka moto au kuuma ambayo huweza kupelekea hali ya kukosa usingizi usiku ambayo mara nyingi hueza kuambatana na hali ya miguu kufa ganzi.
CHANZO CHAKE:
Zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha kuhisi miguu kuwaka moto/ kuuma ambazo hizi huashiria kuathirika kwa mfumo wa nevu ( nerve damage) ama kuathirika kwa mishipa ya damu inayoelekea miguuni.
Sababu hizi ni kama vile:
Ujauzito
Kukoma kwa hedhi ( menopause)
Matumizi ya pombe kupita kiasi
Magonjwa kama vile kisukari
Matumizi ya dawa mbalimbali kama dawa za saratani (Chemotherapy), dawa za kisukari (hasa metformin)
Maambukizi ya virusi vya ukimwi
Upungufu wa vitamini B12 na vitamin B6 kwa uchache
Matatizo ya figo
Kuwa na fangasi wa miguuni (athletes foot)
Kutembea/ kusimama muda mrefu
MATIBABU YAKE:
Kitu cha muhimu cha kufanya ni kuhakikisha kutibu chanzo cha tatizo husika linapolekea miguu kuwaka moto, kufa ganzi au kuuma kama vilivo orodheshwa hapo juu.
Matumizi ya dawa za saratani au kisukari kuweza kusababisha miguu kuwaka moto/ kufa ganzi kama madhara kwa kuwa huzuia kufyonzwa kwa vitamin B12 ambayo hasa husaidia katika kuhakikisha nevu (nerve) zinafanya kazi vizuri.
pamoja vya vyanzo vingine zifuatazo ni njia za kutibu tatizo hili:
tumia kwa wingi vyakula vyenye vitamin B12 kwa wingi kama vile Nyama, samaki, maziwa , mayai au vidonge (supplements) vyenye vitamin B12 kwa wingi.
Tumia dawa za kupunguza maumivu na dawa ya kupunguza kuhisi ganzi kutokana na tatizo la kuathirika kwa nevu, hakikisha umepata ushauri kutoka kwa Mfamasia au Daktari kabla ya matumizi ya dawa hizi.
Loweka miguu yako katika maji ya baridi kwa muda kiasi kila jioni au asubuhi.
Massage miguu mara kwa mara, hii husaidia kuhakikisha mzunguko wa damu kwenda miguuni unakuwa kama unavotakiwa hivyo kupunguza maumivu na hisia za ganzi/ kuwaka moto.
Vaa viatu visivyokubana na kuwa na tabia ya kubadilisha viatu unavovaa mara kwa mara, badilisha soksi mara kwa mara na pia vaa viatu vya wazi katika kipindi cha joto hii yote ni ili kuruhusu miguu kupata hewa ya kutosha.
0 Maoni