FAHAMU DALILI ZA KUOZA MENO



Kwa kawaida meno ni meupe, hayana vitobo na kazi yake muhimu ni kukata, kusaga vyakula na kuweka umbo zuri la mdomo kwa nje na anapotabasamu au kucheka.
TANCDA inaeleza kuwa dalili za meno kuoza ni alama nyeusi sehemu za pembeni au kutafunia, uwepo wa shimo kwenye jino au meno, maumivu ya meno, kuvimba sehemu ya fizi au shavu upande ambao jino au meno yanauma.
Njia za kuzuia kutoboka au kuoza kwa meno ni kupiga mswaki pamoja na dawa mara mbili kwa siku, hasa asubuhi na jioni.
Namna nyingine ni kuhakikisha unaondoa mabaki ya vyakula katikati ya meno kwa kutumia vijiti au uzi na hakikisha unakula mlo kamili.
Wataalamu wa kinywa pia wanashauri jamii kuepuka kuoza au kutoboka kwa meno kwa kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari mara kwa mara na kujenga utamaduni wa kuhudhuria kituo cha afya kwa ajili ya uchunguzi angalau mara moja kwa mwaka.
Kuchunguza afya ya kinywa, hata kama huumwi ni njia ya kubaini mapema matatizo ya meno au fizi na kuchukua hatua kabla ya tatizo kujitokeza. Wataalamu husafisha kinywa kwa kutumia vifaa maalumu vya kuondoa uchafu na kufanya meno na fizi kuwa na afya njema.
Nini kinatokea kama jino likitoboka na kutotibiwa mapema? TANCDA inaeleza kuwa matibabu yasipofanyika mapema mhusika atahisi maumivu, ukakasi au ganzi unapokula vitu baridi au moto, jino linaweza kuvunjika, na hushindwa kutafuna vizuri chakula.
Matatizo mengine yanayoweza kujitokeza ni kutoka usaha kinywani, kutoa harufu mbaya na kupungua kwa ubora wa maisha.usikose somo la mwisho lijalo

Chapisha Maoni

0 Maoni