JINSI YA KUMFANYA MTOTO APENDE VYAKULA VYENYE AFYA


Mara kwa mara wazazi na walezi wengi wamekuwa wakihangaika kuwashawishi watoto wadogo kula vyakula vinavyousadia mwili kuwa na afya nzuri kama vile mboga ambavyo wengi wao huwa hawazitaki.
Ulaji wa vyakula visivyousaidia mwili kiafya mara nyingi huwafamnya watoto wanaoishi maeneo hasa ya mijini kunenepa mwili kupita kiasi na wengine hata kupata maradhi kama vile moyo na kisukari.
Mfano Uingereza kuna idadi kubwa ya watoto wenye matatizo ya afya yanayotokana na uzito wa kupita kiasi - lakini mji mmoja nchini humo unaonekana kufanikiwa kuwasaidia watoto kula vyakula vyenye afya.
Takwimu zilizotolewa kwenye mkutano kuhusu unene wa mwili wa kupindukia zimeonyesha kuwa wa Leeds imeweza kupunguza viwango vya watoto wanene kupindukia kwa 64% katika miaka ya hivi karibuni.
Sehemu muhimu ya mkakati wa mji huo wa kukabiliana na unene wa mwili kupita kiasi ulilenga zaidi shule za chekechea na kuwapatia mafunzo wazazi juu ya nanma ya kuwasaidia watoto wao kuwa wenye afya.
Lakini si kila wakati wazazi na walezi wanaelewa somo la chakula .
CHANZO: BBCSwahili

WASILIANA NA DOKTA HARUNA AKUSAIDIE MASUALA MBALI MBALI YA KIAFYA, MPIGIE SIMU NAMBA 0765 30 33 11

Chapisha Maoni

0 Maoni